Ingawa mara nyingi tumekuwa tukisikia hakuna usalama wa asilimia miamoja kwenye ulimwengu wa kompyuta,ila kinga ni bora kuliko tiba.
Hebu angalia,wengi wetu tumeweka nondo za kutosha majumbani mwetu huku tukiwa na lundo la mbwa wakali. Ingawa vyote hivi sio kama vitawazuia majambazi kukuingilia,ila inaweza kusaidia kuzuia vibaka wadogowadogo.
Kwa mantiki hayo,leo hii tutaangalia njia bora za kujikinga na kujiweka katika mazingira ya usalama.Binafsi nimeshasahau mara ya mwisho ni lini kuvamiwa na virusi au minyoo,sio kwakuwa natumia programu za ulinzi zenye nguuvu saaana au ni bingwa sana kwenye masuala ya kompyuta hadi virusi vinaniogopa,bali ninafuata kanuni bora za usalama wa kompyuta ambazo leo hii nitagawana nanyi. Hivyo bila kupoteza muda hebu tuziangalie kwa mapana yake.
I.Tumia programu unazozihitaji
Wengi tumekuwa wahanga wa matatizo ya kompyuta kwa kujisababishia wenyewe,inawezekana kwa kujua au bila kufahamu.
Kompyuta nyingi zimekuwa zikiathiria na masuala ya kiusalama sio kutoka nje bali ndani ya kompyuta husika. Matatizo haya mengi husababishwa na programu ambazo hazijaandikwa kiusahihi.Chukulia mfano jinsi ukuta wa nyumba unavyoweza kukuangukia na kuvunja vifaa vyako vya ndani au bati ambalo halijagongelewa ipasavyo na kuacha tundu kwenye njia ya msumari na kupitisha maji pindi mvua inaponyesha. Hii ni sawa na hizi programu,kama programu haijaandikwa ipasavyo inaweza kukusababishia matatizo mengi.Sio tu kuhitilafiana na mtambo endeshi(OS) wa kompyuta yako na wewe kuona kama kirusi bali pia inaweza kuacha mianya ambayo wavamizi wanaweza kutumia kuingia kwenye kompyuta yako.
Mazingatio.
1.Ondoa programu ambazo hauzitumii ili kupunguza uwezekano wa matatizo,wengi wetu tumekuwa na mazoea ya kusimika programu nyingi wakati nyingi kati ya hizo huwa hatuzitumii kabisa,hizi programu hujaza nasafi,kuweka uchafu na hatimaye kutuweka hatiani.
2.Hakikisha unatumia programu zilizo kwenye wakati,simika maboresho(update) pindi yanapotokea.Nimeshuhudia watu wengi wamekuwa wagumu kusimika haya matoleo mapya kutokana na hofu mbalimbali.Achana na hofu.Maboresho yanakuja kwa ajili ya mambo mema na si kukudhuru.
Post a Comment