Ni ubunifu mzuri sana ambao
Kwanza unakusaidia kubana matumizi yako ya kwenda kununua kizolea taka
badala yake unatengeneza mwenyewe baada ya kumaliza kutumia kidumu chako
cha mafuta au juice,
Pili kwa wajasiriamali wadogo wadogo wanatakiwa wawe wabunifu kwa kubuni
vitu kama hivi ambavyo gharama yake ni ndogo sana na unaweza ukakuza
mtaji wako,
Tatu kwa kutunza mazingira badala ya kutupa vidumu na kusababisha
uchafuzi wa mazingira wewe unaweza kuvikusanya na kufanya kazi hii huku
mwisho wa siku pesa inaingia mfukoni.
Hivyo ni wakati wako wa kuishughulisha kuliko kukaa bure na kutegemea kusubiri kupata ajira katika ofisi flani ama wizara flani.
Post a Comment