BREAKING NEWS

Category 5

?max-results="+numposts2+"&orderby=published&alt=json-in-script&callback=recentarticles6\"><\/script>");

Category 6

?max-results="+numposts5+"&orderby=published&alt=json-in-script&callback=recentarticles8\"><\/script>");

Category 7

Sunday 23 December 2012

Rwanda kuongoza Afrika kwa Tehama

Rais wa Rwanda,Paul Kagame  
WAKATI anaingia madarakani Machi 24, 2000 kama Rais wa Rwanda, Paul Kagame alitoa ahadi kadhaa kusaidia kukuza uchumi.
Akionekana kufuata misingi ya utawala bora na kujali maisha ya wananchi wake, ahadi nyingi hivi sasa zinatekelezwa kwa vitendo.
Maisha baada ya vita
Chini ya miaka kumi na tano baada ya mauaji ya kimbari yaliyoangamiza watu wengi, miundombinu na hali ya kijamii na uchumi nchini humo,  hivi sasa Rwanda  inaonekana kuja kuwa makao makuu ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) kwa nchi za Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
Wachambuzi wa mambo wanasema pongezi ziiendee mipango mizuri ya Serikali ya kuendeleza miundombinu ya mawasiliano nchini humo, ikiwa ni pamoja na simu za mikononi na mitandao ya ‘ Fibre optic na PC.
Ikiwa imepewa jina la namba moja kwa Tehama kwa nchi za  Afrika Mashariki na Shirika la Biashara na Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNCTAD), Rwanda imefaidika kutokana na vitega uchumi vinavyolenga Tehama kutoka kwa kampuni kubwa za kimataifa kama vile Microsoft, Nokia na Terracom.
Bajeti ya Tehama  ya taifa hilo kwa sasa,  iko sambamba na viwango vya Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), ambalo linaundwa na mataifa tajiri 30, kwa asilimia 1.6, juu ya wastani wa Afrika kwa mbali.
Ikiwa imekabiliwa na uchumi uliozorota, mwaka 2000 Rwanda ilizindua “Dira yake ya mwaka 2020” ili kujenga na kufufua kikamilifu uchumi wa Rwanda, kwa lengo la kuwa na hadhi ya taifa lenye uchumi wa kati     ifikapo mwaka 2020.
Dira ya 2020
Wakati mkakati wa Dira ya 2020 unaangalia kilimo, viwanda, na masuala ya kijamii, ukosefu wa bandari, bei za juu za nauli za ndege na kukosekana kwa utulivu,  kumeifanya Serikali ya Rwanda kuwekeza katika uchumi uliojikita kwenye ICT kama msingi mkuu.
Ikiwa imezindua programu ya utafiti wa kisayansi na elimu, teknolojia na ugunduzi na usambazaji wa mawasiliano, Dira ya 2020 ina lengo la kutoa wanasayansi wenye elimu kubwa na mafundi ili kutimiza haja ya uchumi wa kitaifa,  ambao utaingizwa katika mkakati mkuu wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa ajili ya wakazi wa  Rwanda.
Serikali za nchi  wahisani nazo zimejiingiza pia kwenye behewa la Tehama. Ni mwezi uliopita tu, Idara ya Maendeleo ya Kimataifa ya Uingereza (DFID) ilitangaza ingezindua mradi wa thamani ya pauni 700,000 (dola milioni 1.4) kwa kushirikiana na Serikali ya Rwanda na Benki ya Dunia ,kwa lengo la kufanya ugunduzi katika sayansi na teknolojia na ukuaji wa kiuchumi katika nchi hiyo.
Mtandao wa Maendeleo ya Rwanda, njia ya mtandao ya sekta ya maendeleo ya Rwanda, inaona Tehama  kama dirisha la fursa kufikia hatua ya maendeleo ya viwanda na kubadili uchumi kuwa wa kihabari na maarifa,  ili kuweza kukabiliana kikamilifu na changamoto za maendeleo nchini humo,  na wakati huo huo ikitumia fursa mpya za kiuchumi na kijamii.
Askari 25  waliopokonywa silaha zao, kwa mfano, walipewa vyeti vya ufundi wa kompyuta mwaka 2006 na asasi yenye makao yake mjini Washington DC ya ‘Development Gateway Foundation’.
“Lengo la mafunzo hayo lilikuwa kusaidia kuwafanya askari waliokuwa jeshini kupata kazi za ufundi wa Tehama. Baadhi wameshaanza kushirikiana na kampuni za kutengeneza kompyuta,” anasema Meneja Mradi wa kituo cha mafunzo ya Tehama cha Kanda (RITC) mjini Kigali,  Jerome Gasana. Source:MWANANCHI
 
Copyright © 2013 Ujenzi Online
Share on Blogger Template Free Download. Powered byBlogger