MENO |
Wanasayansi wamekuza jino kutoka kwa mkojo wa binadamu
Matokeo haya yaliyochapishwa kwenye jarida la
utafiti wa kisayansi la Cell Regeneration, yalionyesha kuwa mkojo
unaweza kutumika kuunda celi ambazo zinaweza kutumika kukuza vimelea
vinavyofanana kama meno.Hata hivyo watafiti wa celi za mwili, wanaonya kuwa utafiti huu unakabiliwa na changamoto nyingi.
Vikundi vya wanasayansi kote duniani wanatafuta mbinu za kukuza meno kwa njia ya mahabara ili kukabiliana na tatizo la wazee kung'oka meno na hata wale wanaong'oka meno kutokana na afya mbaya.
Seli zijulikanazo kama -Stem cells - ambazo wanasayansi wanaweza kutumia kukuza aina yoyote ya seli, hutumika sana katika sekta ya utafiti.
Wanasayansi wa China waliofanya utafiti huo, walitumia mkojo wa binadamu, mwanzoni mwa utafiti wao.
Baada ya wiki tatu seli hizo zilianza kufanana kama meno zikiwa na sehemu zote za jino. Hata hivyo meno yenyewe hayakuwa magumu kama meno ya kawaida.
Utafiti huu hata hivyo unahitaji kazi ya ziada ili kuzalisha meno halisi.
Profesa Chris Mason, mwansayansi wa seli za mwili, alisema kuwa mkojo wa binadamu sio hatua nzuri ya kuanzia kutengeza meno halisi.
Sio kiungo kizuri kutumia kwa sababu mkojo hauna seli nyingi na kazi ya kugeuza mkojo kuwa seli ni ngumu sana.
Pia alionya kuhusu tisho la maambukizi kutokana na viini vya bakteria vilivyo kwenye mkojo
SOURCE: BBC SWAHILI
Post a Comment